18 526 678 książek w 175 językach
Jednak się nie przyda? Nic nie szkodzi! Możesz zwrócić produkty nawet do 30 dni
Bon prezentowy to zawsze dobry pomysł. Obdarowany może za bon prezentowy wybrać cokolwiek z naszej oferty.
Kwa zaidi ya miaka kumi na tano vitabu vya mwandishi maarufu kushinda wote katika jamii za Waswahili kote Afrika ya Mashariki na Kati, Marehemu Sheikh Shaaban Robert, havikupatikana Tanzania. Sababu ya kukosekana kwa vitabu hivyo ni kuwa kampuni ya kigeni iliyovichapisha iliamua kuacha kuvichapisha kwa sababu haikulipwa kwa fedha za kigeni jambo, lililosabishwa na hali mbaya ya uchumi. Athari za kupotea kwa vitabu vya Sheikh Shaaban Robert katika miaka hiyo ni kwamba Watanzania wengi hasa wale wenye umri chini ya miaka thelathini, hawamjui mwandishi huyu maarufu na hawakulelewa katika mazingira ya utajiri wa maandishi yake ambayo bila shaka yoyote ni mfano pekee wa utajiri wa urithi wa utamaduni wetu. Kwa kuvichapisha vitabu vya Marehemeu Sheikh Shaaban Robert tunawakaribisha tena Watanzania, hasa vijana kuvisoma, kuburudishwa na kufunzwa na yale aliyoyaandika kwa sanaa na kipaji adimu. In this important work, Shaaban Robert gives guidelines for authors and poets on versification, but also on pre-requisites to good writing.